Duration 1:19

SKULI YA SEKONDARI KIBELE ILIPATA HAMASA ZA KUTOSHA KUTOKA GREEN LIGHT FOUNDATION

Published 26 Oct 2019

Ikiwa ni siku ya Jumatatu ya tarehe 21/10/2019. Taasisi ya Green Light Foundation, ilifunga safari ya kuelekea mkowa wa kusini katika shule ya KIBELE iliopo wilaya ya kati huko Unguja, Zanzibar. Ili kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha Nne na Pili ambao wanakabiliwa na mitihani ya Taifa inayowakumba karibuni.Jambo kubwa katika safari hiyo ni kuwashajihisha wanafunzi ao na kuwapa hamasa zitakazowafanya waweze kufanikiwa katika mitihani yao inayo wakabili. Aidha ziara iyo ni katika kuunga juhudi za serekali ya mapinduzi ya Zanzibar chini ya DR.ALI MOHAMED SHEIN, WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR, TAASISI YA MIMI NA WEWE iliyopo chini ya MH.AYOUB MOHAMMED MAHMOUD. Kuwa Elimu bora kwa mtoto wa kike na mtoto wa kiume inapatikana katika visiwa vya Zanzibar.

Category

Show more

Comments - 0