Duration 2:53

NHC KUJENGA JENGO LA BILIONI 22 MAKAO MAKUU WIZARA YA MADINI

649 watched
0
9
Published 7 Sep 2021

SHIRIKA la Nyumba la Taifa limefungua pazia la ujenzi wa majengo ya kudumu ya makao makuu ya Wizara 24 kwenye Mji wa Serikali maarufu kama Jiji la Magufuli lililopo Mtumba Jijini Dodoma kwa kukabidhiwa ujenzi wa makao makuu ya Wizara ya Madini . Hayo yamebainika leo (Septemba 7, 2021) baada ya Shirika la Nyumba la Taifa kutia saini makubaliano ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Makao Makuu ya Wizara ya Madini utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 22.023 na kukamilishwa ndani ya muda wa miezi 18. Akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, amesema wameliamini Shirika la Nyumba la Taifa kutokana na uzoefu mkubwa lililo nao wa kujenga miradi mikubwa ya kitaifa na kuikamilisha kwa wakati. NHC itatekeleza ujenzi wa makao makuu hayo mapya kwa usimamizi wa Mkandarasi Mshauri wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) ambao ndiyo waliosanifu na kubuni jengo hilo la makao makuu ya Wizara.

Category

Show more

Comments - 1